Msajili wa vyama vya siasa nchini Bw Fransis Mutungi amewataka wananchi wa Mkoa wa Arusha na watanzania kwa ujumla kuepuka kuingiza ushabiki kwenye siasa kwani kufanya hivyo licha ya kuwa chanzo cha kuhatarisha amani wanaharibu lengo la fani hiyo ambayo ina umuhimu na faida kubwa katika jamii kama taratibu na misingi yake ikifuatwa na kuheshimiwa .
Akizungumza
na wananchi na viongozi wa ngazi mbalimbali za Mkoa wa Arusha
waliokusanyika katika uwanja wa Shekh Amri Abeid kuuombea mkoa wa
Arusha amani Bw Mutungi amesema amani ndio msingi wa kila kitu
na haihusiani kabisa na siasa hivyo hakuna sababu ya watanzania
kukubali amani iliyopo ivurugwe na watu wachache wanaosingizia
siasa kwani wanaopenda amani ni wengi kuliko wanasiasa
Wakizungumza
katika hafla hiyo viongozi wa ngazi mbalimbali akiwemo shekh
mkuu wa mkoa shabani bin jumaa na askofu mkuu wa kanisa la
evengelisim centre eliud wamewaomba viongozi wa kisiasa na
wanaotarajia kutafuta nafasi za uongozi kuwajengea wananchi
utamaduni wa kuheshimi sheria na dola iliyoko madarakani
kwani wakizoea kuvunja sheria watafanya hivyo hata uongozi
ulioko madarakani ukibadilika .
Mkuu
wa mkoa wa arusha Bw Magesa Mulongo amesema upo uwezekano wa
kuendesha siasa, kudai haki na hata kukosoa na kutoa
mapendekezo bila kuvuruga amani.
Wananchi
hao wakiwa na viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo wa kisiasa
,viongozi wa dini na wa mila walikusanyika katika uwanja huo
kuhubiri na kuuombea mkoa wa arusha amani unaoandamwa na heka
heka za kisiasa ambazo zimesababisha kuyumba kwa uchumi.
-ITV