o
KIKUNDI cha Al Shabaab kimetishia kumwaga damu zaidi
Kenya kwa kufanya mashambulizi mapya na safari hii wanatamba kupiga patakapouma
zaidi. Kundi hilo limesema kwamba litaongeza idadi ya watu katika kikosi cha
mashambuzi nchini humo kutokana na Kenya kukaidi kuondoa majeshi yake Somalia.
“Tutaishambulia Kenya sehemu itakayowauma zaidi,
tutageuza miji yao makaburi na mito ya damu itatiririka Nairobi nzima,” al
Shabaab ilisema katika taarifa yake na kuongeza:
“Uamuzi wa Serikali ya Kenya kuendelea kuyaacha majeshi
yake Somalia ni ishara ya wazi kwamba, hawajataka kujifunza kutokana na
yaliyotokea katika shambulizi la Westgate,” ilieleza taarifa hiyo huku
ikijigamba kuwa, Kenya itakuwa eneo litakalogubikwa na wingu la damu na vurugu.
Wakati kikundi hicho kikitoa tishio hilo, takriban
miili isiyopungua tisa imepatikana katika eneo la ndani ya kifusi kwenye jengo
hilo, na sehemu ya eneo liliunguzwa kwa moto wakati wa shambulio hilo la
Westgate.
“Baadhi ya miili haiwezi kutambuliwa kabisa na
utambuzi wa vinasaba (DNA) utafanywa ili kutambua, mingine imeharibiwa na
inatisha,” taarifa kutoka Polisi ilieleza.
Hata hivyo haikuwekwa wazi kama idadi ya miili hiyo
tisa imejumlishwa na watu 67 wakiwemo wanajeshi sita waliokufa katika
shambulizi hilo. Rais Kenyatta ajibu Hata hivyo Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta,
juzi alikaririwa akisema majeshi yake yataendelea kubaki Somalia hadi hapo
amani na usalama wa nchi nchi hiyo vitakapotengamaa.
Septemba 21 Shambulio la Westgate lililotokea Septemba
21 mwaka huu katika jengo hilo la maduka ya bidhaa mbalimbali za watu wenye
maisha ya juu, wanadiplomasia na wafanyabiashara wakubwa wa ndani na nje ya
Kenya.
Mbali ya vifo hivyo vilivyofahamika hadi sasa, watu
zaidi ya 170 walijeruhiwa vibaya huku wengine wakipata matatizo ya kisaikolojia.
Miongoni mwa waliouawa ni watoto waliokuwa kwenye tamasha la mashindano ya
kupika kwenye jengo hilo.
Baadhi ya manusura wa shambulio hilo walieleza namna
walivyokutana uso kwa uso na magaidi hao. Kupitia taarifa mbalimbali, magaidi
hao walisikika wakidai wanawasaka Wakenya na Wamarekani ingawa waliouawa na
kujeruhiwa katika shambulio hilo ni pamoja na raia kutoka nchi mbalimbali
ikiwemo Ufaransa, Canada, Australia, Marekani, Uingereza, Ghana na kwingineko.
Pamoja na majeshi na polisi wa Kenya kuzingira jengo
hilo tangu saa chache baada ya tukio, taarifa zinadai baadhi ya magaidi
waliokuwa katika jengo hilo, walitoroka kupitia mtaro wa maji machafu uliokuwa
chini ya jengo hilo na huenda watu wengi zaidi wakawa wamepoteza maisha ikiwemo
mateka waliodaiwa kushikiliwa na magaidi hao ndani ya jengo hilo.
Shambulio hilo ni la pili kwa ukubwa nchini humo
likihusisha kikundi cha al Shabaab chenye ushirika na al Qaeda ambao wanadaiwa
kuhusika na shambulizi kubwa lililotokea mwaka 1998 katika Ubalozi wa Marekani
nchini humo na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 220.

-habarileo