Mtukio ya kikatili yameendelea kushika kasi wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambapo mtoto aitwaye Said Siraji/Said Joshua amelazwa katika Hospitali ya wilaya usiku wa kuamkia leo, baada ya kunusurika kifo katika jaribio la kuchinjwa na baba yake mzazi aliyejulikana kwa jina la Salvatory.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya
wilaya-Kahama; Dakta Joseph Fwoma amesema Siraji amefikishwa hospitalini
hapo leo alfajiri baada ya kuokotwa na wasamaria wema akiwa anakimbia
huko akivuja damu shingoni.
Dakta Fwoma amesema baada ya kufikishwa hospitalini madaktari walimfanyia upasuaji na kumshona sehemu ya koromeo aliyochinjwa na hadi alasiri hii hali yake imeendelea vizuri hasa baada ya kuongezwa damu.
Kwa mujibu wa mama mzazi wa Mariamu Idd(35) amesema, Mtoto Siraji jana alichukuliwa na baba yake mzazi anayeitwa Siraji Salvatory(45) kwenda naye kwake mitaa ya Majengo kwa kuwa wazazi hao walikwisha achana siku nyingi.
Mariam amesema, awali Salvatory alikuwa akimchukua Siraji mara kwa mara na kumpeleka nyumbani kwake na baadaye kumrudisha akidai kuchoshwa na huduma za matibabu kutokana na mtoto huyo kuwa na matatizo ya kiafya.
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga
limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema chanzo cha tukio hilo
inasadikiwa kuwa mtuhumiwa anaugua ugonjwa wa akili.